MALI-USALAMA-HAKI

Wanajihadi kumi na tano wahukumiwa kifo nchini Mali

Kiongozi wa kundi la kijihadi na wapiganaji wengine kumi na wanne wamehukumiwa Ijumaa wiki hii nchini Mali kwa mashambulizi yaliyotekelezwa kusini mwa nchi hiyo, kwenye mpaka wa Côte d'Ivoire na Burkina Faso.

Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine huko Timbuktu, Aprili 2012 (picha ya kumbukumbu).
Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine huko Timbuktu, Aprili 2012 (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / AFPTV / FRANCE 2
Matangazo ya kibiashara

Souleymane Keita, aliyekamatwa mnamo mwaka wa 2016, na washtakiwa wengine wawili waliokuwepo mahakamani, wamehukumiwa kifo, wakati kumi na wawili wengine, ambao hawakuwepo mahakamani, pia wakihukumiwa kifo.

Kulingana na mashahidi ambao walimwona akifika mahakmani, Malian Souleymane Keita, mshtakiwa mkuu, ambaye alikuwa amevaa mavazi meupe, alibaini kwamba yeye sio gaidi, bali ni mwanajihadi.

Mnamo mwaka wa 2013, alishiriki katika shambulio la kundi la Ansar Dine la Iyad Ag Ghali, katika mji wa Konna katikati mwa Mali, shambulio ambalo kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane kiliingilia kati kwa kuwatimuwa wanajihadi hao.

Baadaye, Souleymane Keita aliongoza wapiganaji wa kijihadi ambao waliendesha harakati zao Kusini mwa Mali, kwenye mipaka ya nchi tatu: Mali, Burkina Faso na Côte d'Ivoire. Nia yao ilikuwa kusanikisha tawi la kundi la Ansar Dine katika eneo hilo na kuajiri wanajihadi wapya na kutekeleza operesheni za kijeshi.

Wenzake wawili kutoka Burkina Faso pia walifikishwa mahakamani. Walikiri kufanya mashambulio, hasa katika maeneo mbalimbali nchini Mali, kwenye mpaka na Côte d'Ivoire na Burkina Faso. Wamehukumiwa kwa "ugaidi, kumiliki silaha za kivita, na mauaji". Wote watatu wamehukumiwa kifo.

Wanajihadi wengine kumi na wawili ambao hawakuwepo mahakamni pia wamehukumiwa kifo.