DRC-UCHUMI

Bei ya hati ya kusafiria yapunguzwa nchini DRC

Hati ya kusafiri sasa itatolewa kwa dola 99 za Marekani. Bei hiyo imetangazwa na Wizara ya Mambo ya nje kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha.

Pasipoti ya DRC.
Pasipoti ya DRC. Government of the Democratic Republic of the Congo / Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Hadi hivi karibuni, ilikuwa ni lazima kulipa karibu mara mbili (dola 185) ili kuweza kupata cheti hiki cha thamani.

Raia nchini Jamhurio ya Kidemokrasia ya congo wamekuwa ni wenye furaha baada ya kutangazwa hatua hiyo kushuka kwa bei ya pasi ya kusafiria.

Hata hivyo hii haizuii baadhi kuhoji maswali juu ya mikataba ya umma ya kutengeneza hati hizo za kusafiria. Mkataba mpya ulijadiliwa tena na kampuni ya Semlex kupitia kampuni yake tanzu nchini DRC Locosem.

Mkataba wa awali kabla ya kupata mshirika thabiti, amebaini Nicolas Kazadi, anayesimamia masuala ya miundombinu katika ofisi ya rais wa Jamhuri.

Bado, wengi wanaendelea kujiuliza maswali kuhusu mazungumzo ya kwanza ambayo yameweka bei kubwa kwa pasi hizo za kusafiria, kulingana na ripoti ya mwandishi wetu huo Kinshasa Kamanda wa Kamanda.