DRC-FCC-CASH-SIASA-USALAMA

DRC: Mvutano waendelea kati ya FCC na CASH

Mvutano kati ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Joseph Kabila nchini DRC (FCC) na muungano wa vyama vinavyomuunga moko Félix Tshisekedi ueendelea kushika kasi.

Washirika wa karibu wa Félix Tshisekedi (picha yetu ya kumbukumbu) wanamshtumu Waziri wa Fedha José Yala kususia hatua za rais wa sasa Felix Tshisekedi.
Washirika wa karibu wa Félix Tshisekedi (picha yetu ya kumbukumbu) wanamshtumu Waziri wa Fedha José Yala kususia hatua za rais wa sasa Felix Tshisekedi. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa kisiasa wa rais wa sasa Félix Tshisekedi unataka muungano wa kisiasa kati yake na FCC usitishwe mara moja.

Muungano wa CASH unabaini kwamba vyama vinavyojumuika katika muungano wa Joseph Kabila wa FCC haviruhusu tena serikali ya muungano kufanya kazi kwa utulivu.

Hivi karibuni wahirika wa karibu wa Félix Tshisekedi wamemlenga Waziri wa Fedha, José Sele Yala shughuli. Wanamshutumu mwanachama huyu wa FCC, muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Joseph Kabila, kuzuia mipango kadhaa ya Felix Tshisekedi. Madai ambayo mtuhumiwa amekanusha.

Wakati wa mikutano, kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, washirika wa karibu wa rais wa sasa wanadai kwamba José Yala shughuli huwa akipuuzia hatua za Felix Tshisekedi.

Marcellin Bilomba, mshauri mkuu wa rais Tshisekedi anayehusika na maswala ya uchumi, anataja, kwa mfano, malipo ya wafanyakazi: "Hakulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati. Alipendelea kulipa bili za makampuni ambayo yanamilikiwa na viongozi wake Joseph Kabila na Waziri Mkuu wa zamani Matata Ponyo.

Kwa upande wake José Sele Yala amefutilia mbali madai hayo akibaini kwamba ni madai yasiyokuwa na msingi.

Mvutano kati ya FCC na CASH umeendelea kuuugawanya muungano huu sereikali.