URUSI-SUDAN-USHIRIKIANO-USALAMA

Urusi yathibitisha ujenzi wa kambi kubwa ya kikosi cha majini nchini Sudan

Meli ya kijeshi ya Urusi "Pytlivy" ikivuka Bosphorus kuelekea Mediterranean (picha ya kumbukumbu).
Meli ya kijeshi ya Urusi "Pytlivy" ikivuka Bosphorus kuelekea Mediterranean (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Yoruk Isik

Rasimu ya makubaliano inabaini ujenzi wa kambi kubwa ambayo itachukuliwa kama hifadhi ya vifaa vya jeshi karibu na eneo la Port Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Kituo hiki cha msaada kitatumika kwa shughuli za ukarabati, hifadhi ya vifaa na sehemu ya kupumzika kwa wafanyakazi.

Kremlin imetoa imetoa idhini ya kujenga kambi ya kikosi cha majini nchini Sudan.

Kambi hii itakuwa na uwezo wa kupokea hadi watu 300, raia na wanajeshi, na meli nne za kivita. Kulingana na mpango huo, Urusi itakuwa na haki ya kusafirisha silaha, risasi na vifaa vya uendeshaji wa kituo chake, kupitia bandari na viwanja vya ndege vya Sudan.

Kambi hiyo itakuwa ya kwanza ya aina yake kwa Moscow barani Afrika, na ya pili ulimwenguni, baada ya ile ya Tartus, huko Syria.

Urusi ina ushirikiano wa muda mrefu wa kijeshi na Sudan. USSR iiliagiza silaha kadhaa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan. Biashara hiyo ilipungua baada ya kuanguka kwa Jamhuri ya Kisovyeti, lakini Moscow kutoa ushirikiano wake wa karibu.

Chini ya Omar al-Bashir, Urusi ilishtakiwa kwa kukiuka vikwazo vya silaha.