DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Janga la 11 la Ebola limemalizika

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza rasmi Jumatano kumalizika kwa janga la 11 la Ebola katika historia yake, hali iliyosababisha kutangazwa kwa dharura za kiafya, matumizi ya chanjo na tuhuma za ufisadi kutoka kwa wafadhili.

Kama ilivyo kuwa kwa janga la 10 Mashariki mwa DRC, chanjo ilitolewa kwa "zaidi ya watu 40,580," WHO ilisema. Chanjo iliyotumiwa ilikuwa rVSV-ZEBOV-GP kutoka kwa maabara ya Marekani ya Merck.
Kama ilivyo kuwa kwa janga la 10 Mashariki mwa DRC, chanjo ilitolewa kwa "zaidi ya watu 40,580," WHO ilisema. Chanjo iliyotumiwa ilikuwa rVSV-ZEBOV-GP kutoka kwa maabara ya Marekani ya Merck. REUTERS/Goran Tomasevic/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Jumatano hii, Novemba 18, 2020, ninafurahi kutangaza kwa dhati kumalizika kwa janga la 11 la ugonjwa wa virusi vya Ebola katika mkoa wa Equateur (kaskazini magharibi)", amesema Waziri wa Afya, Eteni Longondo , mbele ya waandishi wa habari wakati ikifikia muda wa mwisho kiafya (siku 42 baada ya mgonjwa wa mwisho kupatikana na virusi vay Ebola).

Kwa jumla, janga hili limeathiri watu 130 (kesi 119 zilizothibitishwa, watu 11 walioshuliwa kuambukizwa) kwa vifo 55, kulingana na takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO).

Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na janga la hapo awali la homa ya kutokwa na damu Mashariki mwa DRC, ambayo ilikuwa bado ikiendelea Juni 1, na kusababisha zaidi ya vifo 2,200 kati ya mwezi Agosti 2018 na mwishoni mwa mwezi Juni 2020, ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika historia ya ugonjwa tangu kugundulika kwa virusi hivyo mnamo mwaka 1976.

Kuanzia Juni 1, DRC ilikuwa bado ikiishi chini ya hatua kali ambazo rais alikuwa amechukua baada ya kesi za kwanza za ugonjwa wa Corona nchini, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo ambayo ilifunguliwa tena mnamo Agosti 15.

Kama ilivyo kuwa kwa janga la 10 Mashariki mwa DRC, chanjo ilitolewa kwa "zaidi ya watu 40,580," WHO ilisema. Chanjo iliyotumiwa ilikuwa rVSV-ZEBOV-GP kutoka kwa maabara ya Marekani ya Merck.