CONGO-HAKI

Familia za vijana waliouawa katika kituo cha polisi Brazzaville kufidiwa

Mahakama nchini Congo imeamua kulipa fidia, hadi faranga milioni 15 za CFA, familia za vijana 13 waliouawa katika kituo cha polisi cha Chacona, huko Brazzaville, usiku wa Julai 22 kuamkia 23, 2018.

Moja ya maneo ya mji mkuu wa Congo, Brazzaville.
Moja ya maneo ya mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rufaa ya Brazzaville siku ya Jumanne ilichunguza rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya mwanzo mwezi Machi 2019, ambayo haikutoa fidia kwa familia zilizofiwa.

Mahakama hiyo ya mwanzo iliwahukumu tu maafisa 6 wa polisi kwa kifungo cha mwaka 1 hadi 3 kwa "mauaji bila kukusudia".

Kulingana na wakili wa familia zilizofiwa, Steve Bagne, majaji wa Mahakama ya Rufaa walibatilisha uamuzi wa kwanza.

Mahakama ilibaini kwamba serikali ya Congo na washtumiwa walifanya makosa na kutrakiwa kulipa fidia ya faranga milioni 15 za CFA kwa kila mwathiriwa.

Baadhi ya familia zilizokuwepo wakati wa kusikiliza hukumu hiyo zimebaini kwamba kiwango hiki cha fedha ni kidogo kwa sababu vijana walipoteza maisha yao mapema.