DRC-USALAMA

Maswali yaibuka kuhusu hatma ya wafungwa waliotoroa jela Beni

Machafuko mapya yametokea katika mji wa Beni, kartika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC. Watu wanane waliuawa siku ya Jumanne Novemba 17 kati ya maeneo ya Oicha na Eringeti. Lakini miili mingine 29 imepatikana tangu Jumatatu, Novemba 16.

Moja ya sehemu ya mji wa BƩni , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Moja ya sehemu ya mji wa BƩni , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. AP Photo/Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Wengi wanajiuliza iwapo miili hii ni ya wafungwa waliotoroka jela hivi karibuni katika eneo la Beni-Kangbayi.

Wafungwa zaidi ya 1,000 walitoroka kutoka gereza la Kangbayi wakati wa shambulizi. Baadhi walichukuliwa kama mateka na kundi la waasi wa Uganda la ADF. Ilidaiwa kuwa walipigwa risasi baadaye.

Kwa mwaka mmoja, na licha ya kuzinduliwa kwa operesheni kubwa kijeshi na jeshi la DRC, FARDC, hali ya usalama haijaboreka katika eneo la Beni, na sasa zaidi ya watu 850 ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida wameuawa, kulingana na vyanzo rasmi kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini.