AFRIKA-UN-UCHUMI-NJAA-USALAMA

UN kupeleka misaada ya dharura ya kibinadamu katika nchi 5 za Afrika

Baa la njaa katika nchi hizi husababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mizozo ya kivita, kuanguka kwa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na janga la Corona.
Baa la njaa katika nchi hizi husababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mizozo ya kivita, kuanguka kwa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na janga la Corona. AP Photo/Marwan Ali

Mark Lowcock, mkuu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, amesema atatumia dola milioni 100 kutoka mfuko wa dharura kusaidia nchi saba kuepukana na baa la njaa.

Matangazo ya kibiashara

Nchi tano zinazolengwa ziko Afrika: Nigeria (milioni 15), Sudan Kusini (milioni 7), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (milioni 7), Burkina Faso (milioni 7) na Ethiopia (milioni 20).

Baa la njaa katika nchi hizi husababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mizozo ya kivita, kuanguka kwa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na janga la Corona.

Kando na bara la Afrika, karibu dola milioni 30 zitatumika nchini Yemen na dola milioni 15 nchini Afghanistan.

Lowcock amesema dola milioni 20 zilizotengwa kwa ajili ya Ethiopia zinatarajiwa kuongezwa.

"Hali ya kurudi mara kwa mara kwa baa la njaa duniani ni aibu katika ulimwengu ambao kuna chakula cha kutosha kwa wote," Bwana Lowcock amebaini .

"Njaa husababisha vifo vya kuumiza na kudhalilisha," ameongeza.

Karibu dola milioni 500 zilitolewa kwa Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura mnamo mwaka 2020.

Mfuko huu unauwezesha Umoja wa Mataifa kujibu haraka dhidi ya migogoro mipya ya kibinadamu au dharura bila kusubiri misaada maalumu.