BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Mmarekani auawa na vikosi vya usalama mbele ya kambi ya jeshi

Raia mmoja wa Marekani ameuawa na vikosi vya usalama mbele ya kambi ya jeshi huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso ambapo wananchi wa taifa hilo wanamchagua rais mpya leo Jumapili, kulingana na vyanzo vya usalama na kidiplomasia.

Askari wa Burkina Faso wakipiga doria karibu na kambi ya kikosi cha jeshi cha RSP, Septemba 29, 2015.
Askari wa Burkina Faso wakipiga doria karibu na kambi ya kikosi cha jeshi cha RSP, Septemba 29, 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

"Ni ajali ya kusikitisha (...) raia huyu wa Marekani alikuwa akitembea mbele ya" kambi ya jeshi ya Baba Sy (katika viunga vya kusini mwa Ouagadougou) na "alishukiwa kuwa ni adui", kilisema chanzo cha usalama kimesema kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

"Kutokana na kuwa alikataa kutii amri, na kujaribu kutimka, (askari) walifyatua risasi hewani za kumtaka asimame, lakini kwa bahati mbaya zilimpata miguuni. Alisafirishwa mara moja katika kituo cha afya ambapo kwa bahati mbaya aliaga dunia, ”kimeongeza chanzo hiki.

Hali ya wasiwasi imetanda nchini, na hasa karibu na kambi na vituo vya jeshi ambavyo mara nyingi hulengwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu katika majimbo mablimbali lakini pia jijini Ouagadougou.