SUDAN-ETHIOPIA-USALAMA

Sudan: ICRC yajaribu kuunganisha tena familia kutoka Ethiopia zilizotengana

Mzozo unaoendelea katika ejimbo la Tigray unasababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalogudumia Wakimbizi, UNHCR.

Wakimbizi kutoka Ethiopia katika kambi ya Fashaga, Sudan, Novemba 20, 2020.
Wakimbizi kutoka Ethiopia katika kambi ya Fashaga, Sudan, Novemba 20, 2020. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Tangu Novemba 10, mzozo wa Tigray umesababisha karibu watu 35,000 kuyatoroka makaazi yaona kukimbialia nchini Sudan.

Kutokana na hofu ya kuuawa katika mapigano hayo, familia nyingi zilitengana baada ya kukimbia hivyo na baadhi kujikuta wako nchini Sudan.

Mzozo kati ya Armenia na Azerbaijan umeendelea kusababisha maafa makubwa, huku kila upande ukiutuhumu mwingine kwa mashambulizi mapya ndani ya jimbo lenye mzozo la Nagorno-Karabakh ambalo limeshuhudia mapigano makali kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Hivi karibuni Azerbaijan na Armenia walitia saini mkataba kamili wa kusitisha mapigano.

Haya yanajiri wakati Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachinian ameomba kuimarishwa kwa uhusiano wa kijeshi kati ya nchi yake na Urusi. Tamko hili linakuja chini ya wiki 2 baada ya jeshi lake kushindwa katika mgogoro wa Nagorno-Karabakh na Azerbaijani, ambayo imeendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.