ETHIOPIA-UN-USALAMA

Addis Ababa yafutilia mbali pendekezo la mazungumzo na viongozi wa Tigray

Guterres, amesema ofisi yake inaguswa na kinachoendelea nchini Ethiopia na kuzitaka pande zinazohasimiana kutafuta suluhu ya Amani.
Guterres, amesema ofisi yake inaguswa na kinachoendelea nchini Ethiopia na kuzitaka pande zinazohasimiana kutafuta suluhu ya Amani. ©REUTERS/Carlo Allegri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka nchi ya Ethiopia, kuruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya raia walionaswa katika mapigano yanayoendelea kwenye jimbo la Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Wito wa katibu mkuu Guterres, umekuja wakati huu Serikali ya Addis Ababa, ikikataa kuketi katika mazungumzo na viongozi wa eneo hilo, ikisema hadi pale itakapohakikisha watawala wa Tigray wamekamatwa.

Guterres, amesema ofisi yake inaguswa na kinachoendelea nchini Ethiopia na kuzitaka pande zinazohasimiana kutafuta suluhu ya Amani.

Haya yanajiri wakati huu maelfu ya raia wa Ethiopia, wanaendelea kukimbilia nchi jirani ya Sudan, huku kila upande unaohusika kwenye mzozo huo ukidai kupata ushindi.

Mashirika ya misaada yanasema imekuwa vigumu kufika kwenye maeneo ya mapigano kutokana na huduma ya mawasiliano pia kukatwa.