ETHIOPIA

Abiy Ahmed katika jaribio la mwisho kuuchukua mji wa Mekele

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Addis Ababa, Ethiopia on December 7, 2019.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Addis Ababa, Ethiopia on December 7, 2019. © Tiksa Negeri / REUTERS

 Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ameagiza jeshi la nchi hiyo kuanza kutekeleza mashambulizi dhidi ya mji mkuu wa Tigray, Mekele, akisema muda wa mwisho waliokuwa wamepewa viongozi wa eneo hilo kujisalimisha umepita. 

Matangazo ya kibiashara

 

Waziri mkuu, Abiy, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Jumapili ya wiki iliyopita, alitoa muda was aa 72 kwa viongozi wa eneo la Tigray kujisalimisha, wito ambao hata hivyo ulipuuziliwa mbali na mamlaka za eneo hilo.

 

Katika taarifa yake, Abiy Ahmed, amesema wakati jeshi likielekea kutekeleza hatua ya mwisho kulikomboa eneo hilo, ameviagiza vikosi vyake kuwa makini ili kuepuka mauaji dhidi ya raia aliosema hawana hatia.

 

Abiy, ameongeza kuwa mamia ya wapiganaji wenye silaha wa Tigray, walijisalimisha kwa vikosi vya Serikali kabla ya muda wa mwisho uliokuwa umewekwa.

 

Haya yanajiri wakati huu raia wa nchi hiyo zaidi ya emfu 40 wameshaingia nchi jirani ya Sudan, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu, yakivituhumu vikosi vya Serikali na vile vya Tigray, kwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia.

 

Ujumbe wa umoja wa Afrika unaojumuisha marais wa zamani, unatarajiwa kukutana na waziri mkuu Abiy Ahmed, kujaribu kumshawishi asitishe operesheni za kijeshi zinazoendelea ili kuruhusu mazungumzo, wito ambao hata hivyo alishaukataa hata kabla ya kukubali kukutana na ujumbe huo.