BURKINA FASO

Roch Christian Kabore, ashinda kiti cha urais kwa muhula wa pili

Le président burkinabè Roch Marc Christian Kaboré, le 28 novembre 2017.
Le président burkinabè Roch Marc Christian Kaboré, le 28 novembre 2017. LUDOVIC MARIN / POOL / AFP

Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kabore, ameshinda muhula wa pili wa urais baada ya kufanikiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura alizotakiwa kupata ili kuepuka kwenda kwenye duru ya pili.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, Kabore, amepata ushindi kwa asilimia 57.87 na kwamba anakuwa rais mteule.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Ahmed Barry, amesema Kabore amefanikiwa kupata idadi ya kura kumuwezesha kushinda katika duru ya kwanza.

Eddie Komboigo, aliyekuwa akigombea kupitia kilichowahi kuwa chama tawala wakati mmoja, ameshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 15.48 ya kura zote, akifuatiwa na Zephirin Diabre, aliyepata asilimia 12.46.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, rais Marc Kabore, amesema ataendeleza mazungumzo na wanasiasa wengine, kwa lengo la kuleta maridhiano na kusaidia vita dhidi ya makundi ya kijihadi.

Rais Kabore, amewataka wapinazani wake kukubali wito alioutoa na kushirikiana nae katika kuijenga Burkina Faso, hasa wakati huu makundi ya kijihadi yakitatiza usalama.