MADAGASCAR

COVID-19 Madagascar: Serikali yafutilia mbali chanjo na kuamua kutumia tiba za kienyeji

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina akizindua dawa ya asili ya kutibu corona mjini Antananarivo tarehe 20 Aprili 2020.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina akizindua dawa ya asili ya kutibu corona mjini Antananarivo tarehe 20 Aprili 2020. © AFP / Rijasolo

Madagascar haitaki kushiriki katika mpango wa kimataifa wa upatikanaji wa chanjo dhidi ya COVID-19, Covax Facility, mara tu ya kurasimishwa na kupitishwa.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ameithibitishia RFI Alhamisi jioni, Novemba 26. Mpango huu uko wazi kwa nchi zote duniani. Kifungu maalum kinaruhusu nchi 92 zinazoendelea, pamoja na Madagascar, kupata kipimo cha chanjo mara tu zitakapowekwa sokoni.

 

Madagascar imejitenga na kupendelea kuwekeza katika dawa ya mitishamba ambayo ilizundua hivi karibuni.

 

"Tulijadili suala hilo Jumanne jioni wiki hii katika kikao cha Baraza la Mawaziri. Bado hatujachukua msimamo juu ya chanjo dhidi ya Corona. Kwa maneno mengine, hatuko kwenye orodha ya nchi zitakazonufaika na chanjo hiyo baadaye, " amesema msemaji wa serikali Lalatiana Rakotondrazafy Andriatongarivo.

 

"Mazungumzo bado yalikuwa yakiendelea siku ya Jumatatu," amesema afisa kutoka wafadhili wa jadi. Tunajua kwamba rais Rajoelina bado anasita kuhusu chanjo hiyo, lakini wasaidizi wake wamekuwa wakijaribu kumshawishi. Wako na chaguo la kuwa kwenye orodha ya walengwa hadi Desemba 7, na kisha kuamuwa ikiwa watabadili msimamo wao. "

 

Wafadhili mbalimbali wamethibitisha taarifa hii: nchi mbalimbali zinaendelea kushinikiza Madagascar kujiunga na mpango huu wa kimataifa.