SUDAN

Sudan: Nani kumrithi Sadeq al-Mahdi kwa kuongoza chama cha Ummah baada ya kifo chake

Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Sudan, Sadeq al-Mahdi, ambaye amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19
Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Sudan, Sadeq al-Mahdi, ambaye amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19 AFP/ASHRAF SHAZLY

Chama cha Ummah kinamsaka kwa udi na uvumba mrithi wa Sadeq al-Mahdi aliyefariki dunia Alhamisi wiki akiwa na umri bwa miaka 85.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka 70 akiwa katika siasa, ikiwa ni pamoja na miaka 56 kama kiongozi wa chama cha Ummah, Waziri Mkuu wa zamani Sadeq al-Mahdi alifariki duni kutokana na ugonjwa hatari wa COVID-19.

 

Kulingana na maafisa kadhaa wa chama chake, itakuwa ngumu kumpata mrithi wa Sadeq al-Mahdi.

 

Kifo chake siku ya Alhamisi nchini Sudan kimeacha pengo kubwa katika chama cha Ummah. Ni miaka kadhaa imepita tangu Sadeq al-Mahdi, atangaze nia yake ya kuachana na siasa lakini hakuwahi kufanya hivyo. Hakuweza hata kumteua mrithi wake, ingawa baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake wanabaini kwamba aliacha wosia. Washirika wake wa karibu wanasema hivi karibuni kamati za chama zitachukuwa uamuzikuhusiana na suala hilo.

 

Wakati huo huo, binti yake Maryam, mmoja wa manaibu viongozi watatu, ameteuliwa kwa muda kuongoza chama cha Ummah.

 

Maryam al-Mahdi, akisukumwa mbele katika siasa na baba yake, anaonekana kuwa mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi.

 

Kaka zake, ikiwa ni pamoja na al-Siddik na Abderrahmane, pia ni miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kuchukuwa uongozi wa chama cha Ummah, lakini uwezekano wa uteuzi wa Abderrahmane umezua utata. Baada ya kuwa mshauri wa Omar al-Bashir, alikataliwa na viongozi kadhaa wa chama. Wengine wanaona, badala yake, kwamba uzoefu huu unamfanya mtu anayefaa zaidi kuchukua uongozi wa chama.

 

Ikiwa chama cha Ummah, kilichoanzishwa miaka 75 iliyopita, kimekuwa kikiongozwa na familia ya al-Mahdi, majina mengine yametajwa kwa kuweza kumrithi Sadeq al-Mahdi. Miongoni mwa majina hayo ni pamoja na al-Wathek Breir, katibu mkuu wa chama na mkwe wa Sadeq al- Mahdi, na Jenerali Fadlallah Nasser, Waziri wa zamani wa Ulinzi na ambaye alikuwa karibu naye sana.