ETHIOPIA-ABIY AHMED

Waziri Mkuu wa Ethiopia aapa kulinda raia huko Tigray

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed. Themba Hadebe/AP Photo

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameahidi leo Ijumaa kwa wapatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) kuwalinda raia kama sehemu ya shambulio katika jimbo la Tigray, ambalo amesema umeingia "katika hatua ya mwisho.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na huduma zake mwishoni mwa mkutano huu, hata hivyo, haionyeshi mazungumzo yoyote yanayowezekana na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF), kinachotawala jimbo hilo la kaskazini mwa nchi.

 

Serikali ilikuwa imetoa muda kwa utawala wa TPLF hadi Jumatano kujisalimisha la sivyo shambulio kubwa litekelezwe na jeshi la Ethiopia dhidi ya mji mkuu wa jimbo hilo, Mekele, mji wenye wakaazi 500,000.

 

Tishio hili limeongeza hofu kwa mashirika ya kibinadamu juu ya hatima ya raia, wakati shambulio la serikali lililozinduliwa Novemba 4 tayari limesababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine kuyatoroka makaazi yao.

 

Waziri mkuu ameahidi "kuwalinda raia," baraza lake la mawaziri limesema katika taarifa yake iliyotolewa baada ya kukutana na Joaquim Chissano, Ellen Johnson Sirleaf na Kgalema Motlanthe, ambao amewashukuru kwa "hekima, ujasiri wao na utayari wao wa kujitolea msaada kwa njia yoyote muhimu".

 

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza mkutano mwingine wowote wa baadaye na wajumbe hao.