JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

CAR: Mahakama ya Katiba yakataa makundi yenye silaha kuwania katika uchaguzi wa wabunge

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin Archange Touadéra.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin Archange Touadéra. REUTERS/Sergei Karpukhin

Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza uamuzi wake kuhusu majina ya watu wanaotaka kuwania katika uchaguzi wa wabunge wa Desemba 27 mwaka huu, uchaguzi ambao utaambatana na uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Katiba imetoa orodha ya majina ya wagombea 1,585 katika uchaguzi wa wabunge, kwa jumla ya viti 140 katika Bunge la Kitaifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

Danielle Darlan, mkuu wa Mahakama ya Katiba, amefutilia mbali watu kutoka makundi yenye silaha kuwania katika uchaguzi wa wabunge.

 

Kulingana na uamuzi wake, watu zaidi ya hamsini kutoka makundi yenye silaha walikataliwa kuwania katika uchaguzi wa wabunge wa Desemba 27.

 

Hali hii huenda ikachochea sintofahamu inayoendelea nchini humo wakati Jamhuri ya Afriika ya Kati ilikuwa inajaribu kuondokana hali hiyo baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko kwa miaka kadhaa, wamebaini wadadisi wa mambo.

 

Desemba 3, Mahakama ya Katiba itatoa uamuzi wake kuhusiana na wale wanaotimiza vigezo vya kuwania katika uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.