BURKINA FASO

Burkina Faso: Kaboré aibuka mshindi, lakini mengi makubwa yamsubiri

Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré.
Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré. LUDOVIC MARIN / POOL / AFP

Baada ya ushindi wake mkubwa, rais Roch Marc Christian Kaboré anakabiliwa na changamoto ya usalama, huku wengi wakijiuliza iwapo ahadi alizozitoa zitatekelezwa.

Matangazo ya kibiashara

Kaboré ambaye alishinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa 57.87% ya kura kulingana na matokeo ya awali, siku za hivi karibu atatawazwa na kuanza rasmi muhula mwingine madarakani.

 

Kuzorota kwa hali ya kisiasa na usalama nchini Burkina Faso kuna hatari ya kuhatarisha ahadi yake wakati wa kampeni: kujenga "Burkina Faso bora kwa watu wote".

 

"Hakuna Matata! Inamaanisha "kila kitu kiko sawa" kwa Kiswahili fasaha. Maneno haya, yalitumiwa sana wakati wa mikutano ya hadhara ya kampeni za uchaguzi wa urais ya hivi karibuni iliyoendeshwa na chama cha MPP, chama madarakani nchini Burkina Faso kwa miaka mitano. Wafuasi wa Kaboré wanasema maneno haya walipelekea rais anayemaliza muda wake kuchukuwa nafasi nzuri.

 

Kila kitu kinaenda sawa kwa Roch Marc Christian Kaboré, ambaye alishinda uchaguzi wa urais wa Novemba 22 katika duru ya kwanza.

 

Baraza la Katiba bado halijatangaza matokeo ya mwisho. Kwaupande wa kambi ya rais, wanasema hawakushangzwa kusikia rais Kaboré anaibuka mshindi katika duru ya kwanza kwa kupata kura nyingi kiasi hicho.

 

Tume ya uchaguzi nchini Burkina Faso, imesema chama tawala cha MPP kinachoongozwa na rais Roch Kabore, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili wiki iliyopita, kimeendelea kushikilia nafasi nyingi bungeni. Chama hicho pamoja na vyama vyake shirika vilishinda takriban viti 90 kati ya 127 katika uchaguzi wa Novemba 22.

 

Chama cha DCP cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Blaise Compaore, aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano dhidi yake mwaka 2014 kimekuwa chama kikubwa cha upinzani bungeni kikiwa na viti 20.

 

Kabore alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Novemba siku ya Alhamisi wiki iliyopita, na kuanza muhula wake wa pili madarakani ambako anakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kupambana na makundi ya wanamgambo.