MALI

Mali: AQMI yatekeleza mashambulizi dhidi ya kikosi cha Ufaransa Barkhane Kidal, Gao na Ménaka

Wanajeshi wa Mali, wakiwa kwenye eneo la Niono.
Wanajeshi wa Mali, wakiwa kwenye eneo la Niono. Jérôme Delay/AP Photo

Mashambulizi kadhaa ya kigaidi, yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la al-Qaeda katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika, yamelenga kikosi cha Ufaransa Barkhane kaskazini mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Duru za kuaminika zinabaini kwamba mashambulizi hayo hayakusababisha hasara kubwa, wala hakuna mtu aliyejeruhiwa au kupoteza maisha, lakini kinachoshangaza ni uratibu wa mashambulizi haya.

 

Miji mitatu, kambi tatu zimekumbwa na mashambulizi hayo: Kidal, Gao na Ménaka. Uvumi umeendelea kuzagaa kwamba hata mji wa Tessalit umeshambuliwa, lakini Barkhane haithibitishi habari hiyo na vyanzo kutoka serikalini vinakanusha habari hiyo.

 

Katika maeneo yote matatu yaliyotajwa, mashambulizi yote yalifanyika kati ya saa 5:30 afajiri na saa 7 (moja) asubuhi leo Jumatatu.

 

Katika mji wa Kidal, makombora mawili, kati ya manane yaliyorushwa, yalililipuka katika kambi ambayo kikosi cha askari wa Ufaransa nchini Mali na katika eneo la Sahel, Barkhane, yanachangia na vikosi vya Umoja wa Mataifa.