WHO-MALARIA

WHO: Vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria, inaelekea kukwama

Mbinu ya kupambana na malaria katika kambi ya nduta
Mbinu ya kupambana na malaria katika kambi ya nduta www.msf.org

Shirika la afya duniani, WHO, limeonya kuwa vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria inaonekana kukwama, wakati huu maelfu ya watu barani Afrika wakiendelea kufa kutokana na ugonjwa hio.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu ugonjwa wa Malaria, WHO inasema idadi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, haijabadilika ukilinganisha na takwimu za mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa shirika hilo, ugonjwa wa Malaria huua watu karibu laki 4 kila mwaka, wengi ni kutoka kwenye mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Ripoti ya WHO, imesema sababu kubwa ya juhudi za kukabiliana na Malaria kuonekana kukwama, kunatokana na nchi wafadhili kupunguza misaada ya kifedha kwa mataifa ambayo bado yanakabiliwa na changamoto ya kudhibiti maambukizi.

WHO kwenye ripoti yakem imeongeza kuwa, usugu wa baadhi ya dawa katika kutibu Malaria, pia kumechangia ongezeko la wagonjwa na vifo.