ALGERIA

Algeria: Rais Tebboune kurejea nchini katika siku zijazo

Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, hapa ilikuwa mwezi Desemba 2019.
Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, hapa ilikuwa mwezi Desemba 2019. Toufik Doudou/AP Photo

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza Jumatatu jioni kuwa atarudi nchini mwake "katika siku zijazo" baada ya kulazwa hospitalini nchini Ujerumani kwa mwezi mmoja akipewa huduma za matibabu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa pendekezo la timu ya matibabu, rais Abdelmadjid Tebboune anaendelea na kile kinachosalia wakati huu akiendelea vizuri kiafya baada ya kutoka hospitali maalum nchini Ujerumani," imesema taarifa fupi kutoka kwa ikulu nchini algeria, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

 

"Rais wa Jamhuri anawahakikishia wananchi wa Algeria juu ya hali yake ya afya, anasema kwamba yuko sawa na kwamba atarudi nchini siku zijazo," imeongeza taarifa hiyo. Hakuna tarehe ya kurudi kwake nchini iliyotangazwa.

 

Bw. Tebboune, mwenye umri wa miaka 75, alilazwa hospitali mnamo Oktoba 28 katika "moja ya hospitali maalumu kubwa zaidi " nchini Ujerumani ".

 

Kabla ya kusafirishwa huko Rhin, alikuwa "alijiweka mwenyewe karantini" kuanzia Oktoba 24 - tarehe ya mwisho alioandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter- baada ya kutangamana na maafisa wakuu katika ikulu ya rais na serikali walioambukizwa virusi vya Corona, na baadae kulazwa "katika kitengo cha utunzaji maalum katika hospitali ya jeshi ya Ain Naâdja huko Algiers.

 

Hii ni taarifa ya kwanza ya afya iliyotolewa na ikulu ya rais wa Algeria tangu Novemba 15.

 

Kukosekana kwa habari ya matibabu kwa wiki kadhaa, na kukaa kwa muda mrefu kwa Bwana Tebboune huko Ujerumani, kumechochea uvumi na mawazo juu ya utawala wa nchi hii kubwa zaidi huko Maghreb, wakati ambapo nchi hii inakabiliwa ongezeko la idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Rais Tebboune anatarajiwa kutangaza Katiba mpya mara tu baada ya kura ya maoni ya Novemba 1 na kufanyia marekebisho Sheria ya Fedha ya mwaka 2021.