MABADILIKO YA TABIA NCHI-BRAZIL

Brazili: Uharibifu wa misitu wa Amazon wachangia katika mabadiliko ya tabia nchi

Misitu ya Amazon ni miongoni mwa misitu iliyoharibiwa zaidi mwaka huu.
Misitu ya Amazon ni miongoni mwa misitu iliyoharibiwa zaidi mwaka huu. AFP Photo/Tarso Sarraf

Uharibifu kwenye msitu wa Amazon nchini Brazil, umeongezeka mwaka huu ikilinganishwa na miaka minane iliyopita, kwa mujibu wa watalaam ambao wanaonya kuwa hali hiyo imechangia pakubwa katika mabadiliko ya tabia nchi.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za watalaam wa kuhifadhi mazingira, imeonesha kuwa ukataji miti kwenye msitu huo ,umeongezeka kwa karibu asilimia 10 katika kipindi cha mwaka moja tu huku karibu maili tano ya msitu ikiwa imeharibiwa hasa katika kipindi ambacho rais Jair Bolsonaro amekuwa madarakani.

Uharibifu huo umuongezeka kutokana na sera zake za kuruhusu shughuli za kilimo na uchimbaji madini maeneo ya misitu.

Aidha utawala wa Bolsonaro, umepunguza ufadhili wa masharika ya kulinda misitu ambayo yamekuwa yakipambana na ukataji miti na ukiukaji wa sheria za mazingira.

Takwimu hizo ni kinyume na malengo ya Brazili ya kuongeza maeneo ya misitu kwa maili 3900 kila mwaka kufikia mwaka huu.

Hata hivyo, rais Bolsonaro ameendelea kupinga takwimu hizo na kusema ni kampeni ya kuuchafulia jina uongozi wake.