UKIMWI

Dawa mpya za HIV waonesha ufanisi kufubaza virusi vya UKIMWI

Siku ya kimataifa ya UKIMWI.
Siku ya kimataifa ya UKIMWI. REUTERS/Francis Mascarenhas

Wakati ulimwengu hivi leo ukiadhimisha siku ya kupambana na viurusi vya Ukimwi, utafiti mpya uliofanywa na Tume ya Umoja wa Mataifa inayopambana na maambukizi hayo, unaonesha kuwa dawa mpya aina ya cabotegravir, ya kupunguza makali ya virusi vya HIV, ambayo imekuwa ikifanyiwa majaribio barani Afrika, inaonesha ufanisi mkubwa hasa kwa wanawake.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umesema kuwa dawa hiyo inayotumika kwa njia ya sindano moja kila baada ya miezi miwili, ina uwezo wa asilimia 89 kuzuia virusi vya HIV kushinda tembe za kumezwa kila siku.

Utafiti huo umebainisha kuwa wanawake wanne waliopewa dawa hizo, waliambukizwa virusi hivyo, ikilinganishwa na wanawke 34 waliopewa tembe za kumeza.

Mkuregenzi wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema kuwepo njia mbadala za wanawake kutoka nchi zenye hatari kubwa ya kuambukizwa, ni njia moja ya kupunguza maambukizi ya virusi hivyo.

Majaribio ya dawa hiyo, yamekuwa yakifanyiKa miongoni mwa wanawake 3200 kutoka nchi za Botswana, Kenya, Malawi, Afrika Kusini, Eswatini, Uganda na Zimbabwe.

Majaribio hayo kwa mujibu wa ripoti hiyo, yalisitishwa mapema kutokana na matokeo yaliyoonesha ubora wa dawa hiyo.