NIGERIA-BOKO HARAM

Nigeria: Boko Haram yakiri kutekeleza mauaji ya wakulima zaidi ya 70

Miili ya watu waliouawa katika shambulio la kundi la Boko Haram juma moja lililopita.
Miili ya watu waliouawa katika shambulio la kundi la Boko Haram juma moja lililopita. RFI Hausa

Kundi la kigaidi la Boko Haram, limekiri kuhusika kwenye shambulizi la wiki iliyopita ambapo wakulima 76 waliwauwa katika vijiji viwili karibu na mji wa Maiduguri, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi iliyopita, watu waliokuwa waliojihami wa bunduki walitumia pikipiki kufanya mashambulizi dhidi ya wakulima waliokuwa wakivuna mpunga katika kijiji cha Zabarmari na baadaye miili 43 ikapatikana na kuzikwa siku moja baadaye.

 

Kupitia mkanda wa video, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, amedai kuwa wapiganaji wake ndio waliohusika na shambulizi hilo.

 

Mauaji hayo yameibua hisia kali miongoni mwa raia wa Nigeria na viongozi, yakitajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miezi ya hivi karibuni.

 

Wabunge wamemtaka rais Mohammadu Buhari kutoa taarifa ya kina kuhusu usalama wa nchi hiyo kufuatia tukio hilo, na kuanzisha uchunguzi wa madai ya ufisadi unaochangia hali ya usalama kuendelea kuwa mbaya Kaskazini mwa nchi hiyo.

 

Tangu mwaka wa 2009 watu zaidi ya Elfu 36 wameuwa na wengine zaidi ya Milioni Mbili wametoroka makaazi yao kutokana na mashamblizi ya mara kwa mara ya Boko Haram, Kaskzini Mashariki mwa nchi hiyo.