ETHIOPIA-UN

UN na Ethiopia wafikia makubaliano kuhusu misaada ya kibinadamu Tigray

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed. REUTERS/Tiksa Negeri

Ethiopia na Umoja wa Mataifa wamefikia makubaliano ambayo yataruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo ya jimbo la Tigray linalodhibitiwa na vikosi vya serikali, ametangaza Ann Encontre, mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) katika kanda hiyo.

Matangazo ya kibiashara

 

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini na waziri wa amani wa Ethiopia, yanatoa ruhusa kwa mashirika ya umoja wa mataifa kufika kwenye mji huo bila vikwazo pamoja na kwenye maeneo jirani ya mji wa Amhara.

 

Hadi sasa mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na wengine maelfu wamekimbilia nchi jirani ya Sudan kutokana na mapigano yaliyodumu kwa majuma takribani matatu.

 

Serikali ilikuwa imekata huduma ya mawasiliano pamoja na kuzuia mashirika ya misaada kufika kwenye êneo hilo, hali iliyofanya kuwa vigumu kupata tarifa kamili ya kinachotokea.

 

Ofisi ya umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada, inasema êneo la Tigray kwa sasa linakabiliwa na uhaba wa chakula, mafuta pamoja na fedha huku shirika la msalaba mwekundu lenyewe likisema kuna uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu.

 

Mwishoni mwa juma lililopita, waziri mkuu Abiy Ahmed, ambaye mwaka jana alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel, alitangaza kumalizika kwa operesheni za kijeshi baada ya kuuchukua mji wa Mekele.