JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Bozizé aenguliwa kuwania urais Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé. REUTERS/Luc Gnago

Mahakama ya Katiba imethibitisha uamuzi wa Tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé , hana nafasi ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 27 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

François Bozizé anashtumiwa mmakosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na mateso bila kusahau vikwazo alivyowekewa na Umoja wa Mataifa.

 

François Bozizé, aliye kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2003 hadi 2013, alitangaza kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi ujao dhidi ya rais anayemaliza muda wake, Faustin-Archange Touadéra.

 

Katika uamuzi wake, Mahakama ya Katiba imeamua kwamba rais huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 74, hatimizi masharti ya "tabia njema" yanayohitajika na Katiba kushiriki katika kinyang'aniro hiki cha urais.

 

François Bozizé, Jenerali wa zamani na mkuu wa zamani wa majeshi aliliondolewa mamlakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi 2013 na waasi wa Seleka, kundi lililoundwa na hasa na makundi ya Waislamu kutoka kaskazini mwa nchi.

 

Bozizé alirudi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa mwaka jana na akatangaza nia yake ya kuwania wadhifa huo mnamo mwezi Julai, akisema uzoefu wake ni muhimu kwa kurudisha amani nchini, ambapo sehemu maeneo mengi yako mikononi mwa makundi yenye silaha.

 

Waranti wa kimataifa wa kukamatwa ulitolewa dhidi yake na mahakama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini amekuwa hana wasiwasi tangu kurudi kwake kutoka uhamishoni.