DRC

Maswali yaibuka kuhusu vifo vya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kinshasa

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi.
Rais wa DRC, Felix Tshisekedi. Reuters/Baz Ratner

Ugonjwa, utunzaji duni wa matibabu, mazingira magumu ya kazi ni miongoni mwa sababu za vifo hivyo, kulingana na chama cha wahadhiri wa UNIKIN.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza chuo kikuu cha UNIKIN kurekodi idadi hii kubwa ya vifo kwa mwaka, hali ambayo inatia wasiwasi katika chuo hiki kikuu.

 

Kinyume na kile baadhi wameendelea kutoa kama sababu, ugonjwa hatari aw COVID-19 sio sababu pekee ya vifo hivyo vingi. Kulingana na chama cha wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kinshasa, inawezekana kuwa wahadhiri sita walifariki kutokana na COVID-19. Wengi wao walifariki wakati jiji la Kinshasa lilikuwa chini ya makataa ya raia kutotembea. Wengine ambao walikuwa wagonjwa hawakuweza kusafiri nje ya nchi, kwani mipaka ilikuwa imefungwa kwa kipndi cha karibu miezi minne.

 

Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kishansa pia wanalalamika juu ya serikali kushindwa kulipia huduma ya matibabu. Isitoshe, taasisi iliyokuwa ikitoa bima ya afya ya pamoja ambayo imekuwa ikilipa bili za dawa haipo tena.

 

Pia kunaripotiwa mazingira magumu ya kazi kwa wahadhiri hawa, ambao wengi wao wana zaidi ya miaka 60. Kuna karibu wahadhiri 1,100 wanaofundisha wanafunzi karibu 30,000 katika Chuo Kikuu cha Kinshasa pekee. Na miongoni mwa wahadhiri hao kuna wale wanaofundisha pia katika vyuo vikuu vingine nchini humo.

 

Mnamo mwezi wa Septemba, wahadhiri hao walipokelewa na rais Félix Tshisekedi, ambaye aliwaahidi kuingilia kati suala hilo ili suluhisho lipatikane. Hata hivyo wahadhiri hao bado wanasubiri.