UN-TABIA NCHI

UN yaona kuhusu kuendelea kuharibiwa kwa mazingira duniani

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. REUTERS/Lisi Niesner

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonya kuhusu uharibifu wa mazingira na uoto wa asili unaofanywa na binadamu, akisema baada ya miaka michache ijayo huenda hali ikawa mbaya zaidi, hukua kibaini kwamba mapambano ya janga la mabadiliko ya tabianchi ni kipaumbele cha juu katika karne ya 21.

Matangazo ya kibiashara

Guterres, amesema ofisi yake inatarajia kuendelea kushinikiza viongozi wa dunia kuja pamoja katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabianchi, ambayo kwa sehemu kubwa imechangiwa shughuli za binadamu.

 

Hata hivyo Antonio Guterres ameikosoa jamii kwa kushindwa kupambana dhidi ya ongezeko la joto duniani na amesema uongozi wa Marekani ni muhimu katika kushughulikia dharura ya mabadiliko ya tabianchi.

 

Bw. Guterres amesema viwango vya joto kali, ukame pamoja na bahari kufikia rekodi za juu za joto zinasababishwa na utunzaji mbaya wa mazingira unaofanywa na mwanadamu, na ametoa wito wa kutokuweko kwa gesi chafu ya kaboni.

 

Amesema makubaliano ya kimataifa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi yasingeweza kufanikiwa bila ushirikiano wa rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, akisema kuwa mkutano wa kilele kati ya Obama na Rais wa China, Xi Jinping ulisaidia kupatikana kwa uungwaji mkono wa China.