DRC

Mzozo wa kisiasa kati ya FCC na CASH wazidi kuibua wasiwasi DRC

Rais wa DRC, Félix Tshisékédi akiwa na rais mstaafu, Joseph Kabila.
Rais wa DRC, Félix Tshisékédi akiwa na rais mstaafu, Joseph Kabila. REUTERS/ Olivia Acland

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mvutano unaendelea kushuhudiwa kati ya muungano wa kisasa wa FCC, wa rais wa zamani Joseph Kabila na ule wa CACH wa rais Felix Tshisekedi.

Matangazo ya kibiashara

Muungano wa FCC unaituhumu ule wa CACH unaoongozwa na rais Thsisekedi kuwa na mpango wa kuwahonga wabunge wa muungano wa FCC ili kumaliza nguvu yake katika Bunge la kitaifa ili kulidhibiti.

Ripoti zinasema kuwa hali imekuwa kwa muda wa siku mbili zilizopita, na sasa uongozi wa Bunge ukiongozwa na spika wa Bunge Jeannine Mabunda, umetoa wito kwa Baraza lenye wazee wenye busara kuchunguza madai hayo.

Aidha, kumekuwa na madai kuwa rais Tshisekedi anataka kuvunja ushirikiano na FCC, muungano alioingia nao kwa makubaliano miaka miwili iliyopita na kuunda serikali.

Baadhi ya wabunge wa FCC wanadaiwa kuwa wamepokea kati ya Dola Elfu Saba hadi Elfu Tisa na tayari wameungana na upande wa rais Tshisekedi.

Hata hivyo, uongozi wa CACH unapinga madai ya kuwahonga wabunge wa FCC na kusema, wale wanaoamua kujiunga na upande wao, wanafanya hivyo kwa hiari yao.