SOMALIA

Donald Trump aagiza wanajeshi wa Marekani kuondoka Somalia

Ndege za kivita za Marekani zikitekeleza mashambulizi ya anga nchini Somalia. Hii ni picha ya maktaba
Ndege za kivita za Marekani zikitekeleza mashambulizi ya anga nchini Somalia. Hii ni picha ya maktaba World Defence Forum/Facebook

Wanajeshi 700 wa vikosi maalum vya Marekani wameshauri jeshi la Somalia kuendelea katika mapambano yao dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wanaohatarisha usalama wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hayo ni baada ya rais wa Marekani kuagiza wanajeshi hao kuondoka nchini Somalia.

 

Uamuzi wa kuondoa askari wa Marekani nchini Somalia ulitangazwa na Pentagon, makao makuu ya jeshi la Marekani Ijumaa jioni. Zoezi hili linatarajia kukamilika mapema mwezi Januari, kabla tu ya kumalizika kwa muhula wa rais wa Marekani Donald Trump.

 

"Marekani haiitengi Afrika wala au kuondoka Afrika," ilisema taarifa ya Pentagon na kuongeza: "Tunaendelea kushirikiana na washirika wetu wa Afrika na kuwapa msaada wa kudumu na kuwaunga mkono. "

 

Washington imeahidi kutoa uwezo wa kuendesha shughuli za kukabiliana na ugaidi nchini Somalia. Jeshi la Marekani litaendelea kuwa na kambi zake nchini Kenya na Djibouti, ambapo kunapatikana ndege zake zisizo na rubani zinazoendesha mashambulizi nchini Somalia.

 

Kulingana na wizara ya Ulinzi, sehemu moja ya wanajeshi 700 wa Marekani waliotumwa nchini Somalia watapelekwa mbali kidogo na Afrika Mashariki na wengine watapiga kambi karibu na kanda hiyo.

 

Lakini kuondoka kwa wanajeshi wa Merika, jeshi la Somalia hata hivyo halitapata mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na vikosi maalum vya Marekani.

 

Tangazo la kuondoa wanajeshi hao wa Marekani nchini Somalia linaja siku chache baada ya kifo cha afisa mmoja wa CIA, mmoja wa askari wa kitengo kikosi maalum, aliyeuawa katika vita nchjini Somalia.

 

Tangazo hili linatolewa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa wabunge nchini Somalia. Wataalam wana hofu kwamba huenda mashambulio ya kigaidi yakaongezeka wakati wa kampeni za uchaguzi.