DRC-SIASA-TSHISEKEDI-KABILA

Muungano wa FCC-CACH wavunjika DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi Sumy Sadurni / AFP

Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi ametangaza kumalizika kwa muungano wa kisiasa kati ya FCC na CACH, miungano miwili iliyokuwa inaunda serikali ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ametangaza hatua hiyo Jumapili Desemba 6 katika hotuba ya dakika thelathini ambapo pia alitanga ripoti kuhusu matokeo ya mashauriano ya kitaifa ya mwezi wa Novemba.

"Ndugu zangu wananchi, nimewashauri, mliniambia mengi, "alisema rais wa DRC wakati wa hotuba iliyohitimisha wiki kadhaa za mashauriano ya kitaifa.

Alitaja maswala na mapendekezo ambayo yalitoka kwa mashauriano ya kitaifa.

Kukosekana kwa utulivu, ukosefu wa usalama, utawala wa kidemokrasia, ufisadi, ajira kwa vijana na nafasi ya wanawake, orodha ni ndefu sana, lakini "mengi yamezingatiwa," amebaini rais Tshisekedi.

Kilichowekwa mbele kulingana na rais Tshisekedi katika wiki za hivi karibuni ni kukataliwa kwa muungano wa serikali FCC-CACH, unaoundwa pamoja na kambi ya mtangulizi wake Joseph Kabila.

"Hainiruhusu kutekeleza mpango wangu na kufikia matarajio ya Wacongo," amesema Félix Tshisekedi. Amezungumzia pia hali ya "mgogoro unaoendelea" na vizuizi vya bunge, akitoa mfano wa hivi karibuni wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Katiba.

Wakati huo hio rais Tshisekedi amesema atateua afisa atakayehusika na kutambua muungano mpya wa serikali katika wabunge. Katiba, ambayo inatoa uwezekano huu, inabainisha kuwa ujumbe wa kutafuta ukweli unachukua muda wa siku 30, unaoweza kuongezwa mara moja.

Walakini kwa upande wa Lambert Mendé, mbunge wa kitaifa kutoka muungano wa FCC, afisa huyo anaweza kuteuliwa tu kama Waziri Mkuu hayupo.

Ikitokea mpango wake huo utashindwa, rais wa DRC atatoa uwezekano wa kulivunja Bunge: "Nitatumia uwezo ninaopewa na Katiba, ili ni rurudi kwenu, wananchi, na kuwaomba wingi huu katika Bunge, "amesema rais Tshisekedi, huku akibini kwamba njia hiyo itakuwa suluhisho la mwisho.