GHANA-SIASA-UCHAGUZI-MATOKEO

Ghana yasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais, watano wauawa tangu Jumatatu

Wagombea wakuu wa urais nchini Ghana John Mahama (Kushoto),  na rais John Akuffo Addo
Wagombea wakuu wa urais nchini Ghana John Mahama (Kushoto), na rais John Akuffo Addo venturesafrica

Raia wa Ghana wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Jumatatu wiki hii, huku ikidaiwa kuwa watu kadhaa waliuawa.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Ghana uchaguzi huo wa urais na wa wabunge uligubikwa na vurugu ambazo zilisababisha vifo vya watu 5 na 17 kujeruhiwa tangu Jumatatu, wakati wagombea wawili wakuu wanaendelea kila mmoja kubaini kwamba ameshinda uchaguzi huo.

Tangu siku Jumatatu wiki hii (siku ya kupiga kura), "visa 21 vinavyohusiana na vurugu vimeripotiwa katika uchaguzi huo, " polisi ya Ghana imesema katika taarifa na kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Matukio sita kati ya haya yanahusiana na milio ya risasi, vifo vya watu watano na 17 kujeruhiwa.

Vurugu hizo ziliibuka Jumatatu, siku ya uchaguzi, na Jumanne, wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea katika mikoa tofauti nchini.

Tume ya uchaguzi ya Ghana limetoa wito kwa wananchi kuwa na subira na ilitangaza matokeo kutoka mikoa 7 kati ya 16 ya nchi hiyo, huku mgombea wa upinzani John Mahama akingoza dhidi ya rais anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo, ambaye anawania muhula wa pili.