GHANA-SIASA-UCHAGUZI

Ghana: Upinzani haukubalini na ushindi wa Nana Akufu-Addo

Rais mteule wa Ghana  Nana Akufo-Addo
Rais mteule wa Ghana Nana Akufo-Addo REUTERS/Francis Kokoroko

Kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi Jumatano wiki hii jioni, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amechaguliwa kwa muhula mwingine baada ya kura zake na zile za mpinzani wake mkuu kukaribiana.

Matangazo ya kibiashara

Mpinzani wake wa kihistoria John Mahama bado hajazungumza. Mbunge aliyechaguliwa kutoka chama chake alitangaza Jumatano usiku kwamba upinzani umefutiliwa mbali matokeo ya uchaguzi na unatarajia kukata rufaa juu ya uamuzi wa Tume ya Uchaguzi.

Wakati wafuasi wa rais anayemaliza muda wake walimiminika mitaani katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kusherehekea ushindi wa Nana Akufu-Addo, mbunge wa chama cha NDC cha John Dramani Mahama alitangaza mbele ya  waandishi wa habari kwamba chama hicho kimekataa kukubali kushindwa.

Alitishia kupinga matokeo haya ya uchaguzi mbele ya mahakama. Alisema kuwa katika siku zijazo, ushahidi wa udanganyifu utatolewa, kulingana na mwandishi wetu maalum huko Accra, Christina Okello.

Kwa upande wake, John Dramani Mahama hajajibu na amejizuia kupiga simu, kumpongeza Nana Akufo-Addo kwa ushindi wake. Katika hotuba yake ya mwisho, siku ya Jumanne, John Mahama alionya kwamba "atapinga jaribio lolote la udanganyifu wa kura", wakati uvumi kwamba alikuwa amekubali ushindi huo, ulisambazwa kwa masaa kadhaa kwenye mitandao ya kijamii.