AFRIKA KUSINI-COVID 19

Covid-19: Afrika Kusini yakabiliwa na mlipuko wa pili wa maambukizi

Watalaam wa afya walio kwenye mstari wa mbele kupambana na janga la Corona
Watalaam wa afya walio kwenye mstari wa mbele kupambana na janga la Corona REUTERS

Afrika Kusini imeathirika zaidi barani Afrika na janga la COVID-19 na imepitisha idadi ya visa vipya 6,000 kwa siku, ameonya Waziri wa Afya wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo  inakabiliwa na mlipuko wa pili wa virusi vya Corona mamlaka nchini humo ilisema Jumatano jioni.

Afrika Kusini ilirekodi visa vipya 6,709 Jumatano pekee na vifo 135 katika muda wa saa 24 zilizopita. Waziri wa Afya Zweli Mkhize ameelezea wasiwasi wake.

Idadi ya visa vipya imekuwa ikiongezeka sana kwa siku kumi, na kuashiria mlipuko wa pili wa virusi vya Corona, hasa Kusini mwa nchi, katika mkoa wa Cape, lakini pia Kusini-Mashariki, na mkoa wa Pretoria na Johannesburg.

Tofauti na mlipuko wa kwanza, vijana ndio wanaathiriwa zaidi, hasa watoto wa miaka 15-19. Mwaka wa shule nchini Afrika Kusini umefikia tamati na likizo ya majira ya joto imeanza, na hivi karibuni kutakuwa na sikukuu nyingi.

"Maambukizi yanasambaa haraka" ameonya waziri wa afya, "vijana wengi wameonesha dalili za maambukizi ya virusi vya Corona, na wamekuwa wakiambukizana bila kujua".

Kwa sasa, hakuna swala la watu kutotembea, lakini mamlaka zinatoa wito kwa wananchi kuwajibika wakati wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.