GHANA-SIASA-UCHAGUZI

Ghana: Mgombea wa upinzani John Dramani Mahama akataa kukubali kushindwa

John Mahama mgombea urais wa upinzani nchini Ghana aliyekataa kutambua matokeo ya Uchaguzi wa urais
John Mahama mgombea urais wa upinzani nchini Ghana aliyekataa kutambua matokeo ya Uchaguzi wa urais ittelecomdigest.com

Rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama amefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayompa ushindi mpinzani wake, rais anaye maliza muda wake Nana Akufo-Addo.

Matangazo ya kibiashara

Nana Akufo-Addo alichaguliwa tena kwa muhula wa pili kama rais wa Ghana kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi.

Chama chake kilikuwa tayari kimetangaza kwamba kinafutilia mbali matokeo ya uchaguzi lakini John Dramani Mahama alikuwa bado hajazungumza.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii, John Dramani Mahama alitaja matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa ya udanganyifu na kutishia kuchukua "hatua zote za kisheria kuondoa udhalimu huu."

"Tumeona tangu Jumatatu, Desemba 7, 2020 kwamba hatua nyingi zilichukuliwa kwa kuiba kura kwa niaba ya rais anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo, ambaye pia ana udhibiti au ushawishi kwa Serikali na taasisi zake, "John Dramani Mahama amesema.

Licha ya juhudi kubwa za chama tawala kutoa rushwa kwa wapiga kura, kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana nchiniGhana, watu walielewa ni nini kilikuwa hatarini, na ilikuwa wazi kutokana na matokeo yaliyoonyeshwa kisheria kwamba chama cha Democratic National Congress kiilishinda uchaguzi wa urais na wa wabunge. Hakuna udanganyifu, wizi wa kura au uwongo utakaofuta ukweli huu, " amesema rais huyo wa zamani wa Ghana

Kulingana na Tume ya Uchaguzi, Nana Akufo-Addo, kiongozi wa Chama cha New Patriotic Party (NPP), ameshinda kwa 51.59% ya kura dhidi ya 47.36% alizopata John Dramani Mahama. Takwimu zilizokataliwa na mgombea wa upinzani wa National Democratic Congress (NDC). "Wapiga kura wa Ghana walipiga kura kwa ajili ya mabadiliko," amesema.