MAREKANI-ETHIOPIA-TIGRAY

Marekani yasahihisha madai ya uwepo wa wanajeshi wa Eritrea Tigray

Wapiganaji wa eneo la Tigray nchini Ethiopia
Wapiganaji wa eneo la Tigray nchini Ethiopia France24

Marekani imesema ina imani na ripoti inayodai Eritrea inahusika kijeshi katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, kulingana na shirika la habari la REUTERS likimnukuu msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo serikali za Ethiopia na Eritrea zimeendelea kukanusha madai hayo zikibaini kwamba ni madai yasiyo kuwa na msingi.

"Tumepokea ripoti za kuaminika juu ya ushiriki wa jeshi la Eritrea huko Tigray na tunaona hii kama hatari kubwa.

Tunashauri wanajeshi hawa waondolewe mara moja," msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani ameongeza.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa, wiki hii ulitangaza makubaliano mapya ya kibinadamu na serikali kuu ya Ethiopia.