MOROCCO-ISRAEL-DIPLOMASIA

Morocco na Israeli zafufua uhusiano wao

Mfalme Mohammed wa Morocco akiwa na famiia yake pamoja na wageni, hivi karibuni
Mfalme Mohammed wa Morocco akiwa na famiia yake pamoja na wageni, hivi karibuni Moroccan Royal Palace / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba Morocco imekubali kurekebisha uhusiano wake na Israeli, kabla ya kuthibitishwa na Rabat.

Matangazo ya kibiashara

Trump pia amebaini kwamba alisaini tangazo linalotambua umiliki wa Morocco kwa eneo lililojitenga la Sahara Magharibi.

Alhamisi hii, Desemba 10, mahojiano ya simu kati ya Donald Trump na Mohammed VI yalionekana kuzaa matunda. Rais wa Marekani alimtangazia mfalme wa Morocco kuwa Marekani imeamua kutambua uhuru wa Morocco kwa eneo la Sahara Magharibi, na kufungua ubalozi katika mji wa Dakhla.

Mohammed VI, kwa upande wake, alionyesha kwamba nchi yake itaanza tena uhusiano wa kidiplomasia na Israeli, ameripoti mwandishi wetu huko Casablanca, Nina Kozlowski. Mfalme Mohammed VI alisema yuko tayari kuruhusu safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili na kukuza uhusiano wa kiuchumi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco, kwa upande wake, imetangaza kufungua tena ofisi ya uhusiano wa kidiplomasia na Israeli, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya uhusiano na serikali ya Kiyahudi hayatakuwa na madhara kwa Palestina.

Morocco inakuwa nchi ya nne ya Kiarabu kurejesha tena uhusiano na Israeli.