DRC-SIASA-SPIKA

Spika la Bunge la DRC, Jeanine Mabunda, ang'olewa mamlakani

Jeanine Mabunda aliyekuwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyeondolewa katika nafasi hiyo 10/12/2020
Jeanine Mabunda aliyekuwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyeondolewa katika nafasi hiyo 10/12/2020 Assemblée Nationale/twitter.com

Kufuatia mvutano na vurugu vilivyojitokea mapema wiki hii katika Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, suluhu imeanza kupatikana baada ya wabunge kupiga kura ya kung'oa kwenye wadhifa wake spika wa bunge Jeanine Mabunda.

Matangazo ya kibiashara

Hatu hii imekuja siku kadhaa baada ya mpasuko kujitokea katika muungano wa kisiasa, ambao rais Felix Tshsekedi alibaini hivi karibuni kwamba ndio ulisababisha kuzorota kwa shughuli za serikali, kabla ya kutangaza siku ya Jumapili kuuvunja muungano huo uliokuwa unaundwa na miungano ya FCC na CASH.

Jeanine Mabunda ni mmoja wa vigogo wa muungano wa FCC wa aliyekuwa rais wa DRC, Joseph Kabila.

Wengi wanaamini kwamba Joseph Kabila Kabange bado alikuwa na ushawishi katika serikali ya DRC kutokana na kuwa muungano wake ulikuwa wingi wa viti katika Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti.

Jeanine Mabunda ameondolewa kwene wadhifa wake kwa kura 281kwa jumla ya wabunge 484.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais Félix tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge ili apate wingi wa wabunge ambalo kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya wabunge kutoka chama cha mtangulizi wake rais mstaafu Joseph Kabila.