COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d’Ivoire kutoa chanjo kwa 20% ya raia wake

Upimaji wa maambukizi ya virusi vya Corona
Upimaji wa maambukizi ya virusi vya Corona Steeve Jordan / AFP

Pamoja na visa visivyo pungua 22,000 vilivyoripotiwa tangu kuzuka kwa janga la COVID-19 na vifo 133 kuthibitishwa, Côte d'Ivoire inaonekana kuepuka janga hilo, ikilinganishwa na nchi zingine hata

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Côte d’Ivoire inajiunga na mpango wa Covax na itazindua kampeni kubwa ya chanjo mwaka ujao serikali ilitangaza wiki hii.

Raia milioni tano wa Côte d’Ivoire watapewa chanjo kuanzia mwezi Aprili 2021, bila malipo, msaada uliotolewa na mpango wa kimataifa wa Covax ambao unakusudia kutoa chanjo dhidi ya COVID-19 kwa kiwango kikubwa katika nchi zinazoendelea kwa kutoa zaidi ya dozi bilioni moja kwa jumla.

Kama inavyopendekezwa na shirika la Afya Duniani, WHO, Cote d'Ivoire itatoa chanjo hiyo kwanza kwa wafanyakazi wa afya, vikosi vya ulinzi na usalama na pia walimu.

Halafu awamu ya pili itawalenga watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walio na magonjwa sugu. Mwishowe, chanjo hiyo itatolewa kwa wasafiri wanaotoka na kwenda katika nchi za kigeni.

Chanjo hii itakayotolewa iliyotengenezwa na maabara ya Pfizer-BioNTECH na Moderna.