CHAD-SIASA

Chad: Maaskofu waonya kuhusu mizozo kati ya wafugaji na wakulima

Rais wa Chad Idriss Déby Itno
Rais wa Chad Idriss Déby Itno RFI

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Chad wametoa wito kwa rais wa nchi hiyo  Idriss Deby,kuingilia kati kumaliza migogoro kati ya wafugaji na wakulima ambayo imesababisha vifo vya watu wengi tangu kuanza kwa msimu wa mavuno, miezi miwili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Uhasama huo kati ya wakulima na wafugaji nchini Chad umedumu miaka kadhaa na unadhoofisha utulivu na amani kati ya jamii za wafugaji na wakulima bila hata hivyo mamlaka kuingilia kati kukomesha vurugu hizo.

Kwa miezi miwili, machafuko kati ya jami hizi mbili yamekuwa yakijirudi kila kukicha. Shamba lililokuwa linalosubiri kuvunwa liliharibiwa na mifugo, na kusababisha vita kati ya wakulima na wafugaji.

Kulingana na Askofu Séverin, katibu mkuu wa Barazala ku la Maaskofu nchini Chad, silaha za vita hutumiwa katika mapigano kati ya jamii hizi mbili:

"Kuna watu ambao hutumia bunduki  za aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kalashnikov, Famas, ni hali ya inatisha.

Tumeshuhudia majeruhi katika vituo vyetu vya afya. Watu wanaokufa ambao wamejeruhiwa ni raia wa Chad, " amesema Askofu Séverin.

Sababu zote zimechunguzwa, bila kupata majibu. Hata hivyo wakulima na wafugaji ni 80% ya raia wa Chad.

Wasiwasi ni kuona mzozo huu utaendelea kushika kasi. Hii ndio sababu maaskofu ameamua kutoa wito kwa rais Idriss Deby.

Kulingana na wataalamu, mzozo kati ya wafugaji na wakulima tayari umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 nchini kote Chad.