DRC-FCC-KABILA

DRC: FCC yadai kupoteza na kufikiria kujijenga upya

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, ambaye ni kiongozi wa muuungano wa kisiasa wa FCC
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, ambaye ni kiongozi wa muuungano wa kisiasa wa FCC Reuters

Muungano wa vyama vya kisiasa wa FCC wa aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila Kabange umekiri kuwa kung'olewa kwa Jeanine Mabunda kwenye wadhifa wa spika wa Bunge la nchi hiyo ni vita kubwa ambapo ulipoteza nafasi muhimu.

Matangazo ya kibiashara

Muungano wa FCC ulioanzishwa na Joseph Kabila umetoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kufunga vibwebwe, wakati wengi wanaendelea kujiuliza maswali kadhaa kuhusu hatma ya FCC.

Baada ya Jeanine Mabunda kutimuyliwa mamlakani na kuvunjwa kwa ofisi ya Bunge (kuondolewa kwa wajumbe 5 kati ya 6 wa kamati kuu ya Bunge), PPRD, chama cha Joseph Kabila, hatimaye kimekiri kushindwa.

"Ushindi hauji kila wakati. Wacha tu tufikirie haraka jinsi ya kuimarisha muungano wetu. Maumivu ni makubwa, lakini tusikati tamaa. Wacha tuendelee na vita hivi, wanaharakati wapendwa, ”chama cha PPRD kimeandika kwenye mitandao yake ya kijamii.

Patrick Nkanga, mmoja wa makada wa chama cha PPRD, amebaini kwamba wakati umewadia wa kufanya mabadiliko makubwa kwa chama cha PPRD na pia kwa muungano wa FCC. Hii sio mara ya kwanza tunakumbwa na hali hii, huku wafuasi wengine kadhaa wa FCC wakimuunga mkono.

Suala la mabadiliko liliibuka mnamo mwaka 2018 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais. Muungano wa kisiasa upo, lakini umedhoofishwa. Inabakia kuona jinsi ya kurekebisha muungano huo na kupata wanasiasa waliopevuka.

Baadhi wanasubiri kuanzishwa haraka kwa mchakato ili muungano wa  FCC uweze kukabiliana na hali mpya ya kisiasa, changamoto mpya na matarajio ya raia.

Baadhi ya maafisa wa FCC wanabaini kwamba mratibu na viongozi wa muungano huo wabadilishwe baada ya muungano wa FCC kushindwa mara mbili.

Viongozi hao wamekuwepo kwa miaka kadhaa na hakuna maendeleo yoyote, waziri kutoka muungano wa FCC amesema.