MOROCCO-ISRAEL-UN

Sahara Magharibi: Umoja wa Mataifa wasalia kimpya baada ya tangazo la Trump

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa RFI

Hakuna majibu kutoka kwa upande wa Umoja wa Mataifa baada ya Marekani kutangaza kwamba inatambuwa uhuru wa Morocco kwa Sahara Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Saa chache baada ya tangazo hilo la Marekani,  Morocco imethibitisha kwamba inatambua uhalali wa nchi ya Israeli.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia hajawahi kujibu, mwezi uliopita, kuhusu uvamizi wa Rabat katika eneo lililo chini ya kikosi cha Umoja wa Mataifa katika eneo hilo linalozozaniwa kati ya Morocco na  Chama cha Polisario (MINURSO).

Hata hivyo, Chama cha Polisario Front kimefutilia mbali uamuzi huo wa Marekani, kulingana na Oubi Bouchraya Bachir, mwakilishi wa chama hicho barani Ulaya na Umoja wa Ulaya.

Ni uamuzi unaokwenda kinyume na usalama na utulivu wa kikanda [...] ambao kwa hakika utakuwa na athari mbaya kwa juhudi za Umoja wa Mataifa za kutafuta suluhisho la mzozo huo, " alisema Oubi Bouchraya Bachir.

Wakati mapigano yameanza kurindima tena tangu mwezi uliopita katika eneo la Sahara Magharibi, Morocco inaonekana kupata ushindi wa kidiplomasia wa kiwango cha juu wa utambuzi wa Marekani kuhusu uhuru wake kwa eneo hilo.

Msimamo huu wa Marekani ni uungwaji mkubwa wa kidiplomasia kwa Rabat lakini ni msimamo ambao unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa Umoja wa Mataifa.