BURKINA FASO-SIASA

Kesi ya Norbert Zongo: François Compaoré kurejeshwa nyumbani kusikilizwa

Francois Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré
Francois Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré Photo: Ahmed Ouoba/AFP

 Ingawa Ufaransa, mnamo mwezi Februari, iliidhinisha kurudishwa kwa François Compaoré nchini Burkina Faso, kaka wa rais wa zamani bado hajarudi nchini humo. Mawakili wake wamewasilisha rufaa kwa mamlaka nchini Ufaransa.Utangazaji

Matangazo ya kibiashara

Ni miaka 22 Jumapili hii, Desemba 13 tangu Norbert Zongo auawe huko Sapouy, katikati-mashariki mwa Burkina Faso. Wakati huo mwandishi wa habari huu alikuwa akichunguza kifo cha David Ouedraogo, dereva wa François Compaoré, kaka wa rais wa zamani Blaise Compaoré.

Baada ya miaka kadhaa kusimama, kesi iyo ilirejelewa upya baada ya mapinduzi ya mwaka 2014.

Rufaa ya utetezi wa François Compaoré itachunguzwa mnamo Desemba 18 na mamlaka nchini Ufaransa. Kwa upande wa mawakili wake wamesema, kurudishwa kwa mteja wao nchini Burkina Faso ni kinyume cha sheria. Upande wa utetezi umetoa hoja kadhaa.

Kwanza, François Compaoré hajawahi kushtakiwa nchini Burkina Faso. Pili, usalama wake na wa mawakili wake uko hatarini nchini Burkina Faso.

Katika miaka ya hivi karibuni Waziri wa Sheria nchini wa Burkina Faso, René Bagoro, aliviambia vyombo vya habari kwamba tayari barua imeandikwa kuelekea nchini Ufaransa kuwaomba viongozi wa Ufaransa kumrejesha mtuhumiwa huyo ili ahukumiwe nyumbani.

Wakili wa François Compaoré, Pierre Olivier amesema kwa sasa mteja wake yupo huru licha ya kwamba hawezi kuondoka nchini Ufaransa, wanachosubiri ni serikali ya Burkina Faso kueleza anarejeshwa nchini humo kwa misingi gani.

François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, alikamatwa mnamo Octoba 29 katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris, kwa mujibu wa wakili wake, Pierre-Olivier.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa ilitolewa na mahakama ya Burkina Faso kuhusiana na uchunguzi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo mwaka 1998.

Mwili wa mwandishi wa habari Norbert Zongo na wenzake watatu ulikutwa umechomwa moto ndani ya gari mnamo mwezi Desemba mwaka 1998 wakati alikuwa akifanya uchunguzi kuhusu kifo cha David Ouedraogo, dereva wa François Compaoré.