MSUMBIJI-UGAIDI

Ugaidi: Ureno kutoa msaada wa vifaa kwa Msumbiji

Ramani ya nchi ya Msumbiji
Ramani ya nchi ya Msumbiji RFI

Ureno itatuma ujumbe na vifaa vya kijeshi kwa Msumbiji, nchi rafiki, iliyokumbwa na mzozo mkubwa uliosababishwa na magaidi wenye msimamo mkali wa Kiislamu kutoka kundi la al-Shabab, ambalo lina mafungamano na kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Uasi kaskazini mwa Msumbiji ulianza mnamo mwaka 2017.
Utangazaji

Kuanzia mwezi Januari 2021, wanajeshi wa Ureno watasafiri kwenda Msumbiji kuanzisha mpango wa mafunzo kwa jeshi la Msumbiji.

Vikosi vya majibu ya haraka, vikosi vya anga na ulinzi wa mashambulizi ya kimtandao vitahusika katika mafunzo haya.

Kuanzia majira ya joto Ureno iliitikia vyema wito wa Maputo wa msaada katika kupambana na kundi la kigaidi lenye mafungamano na IS, al-Shabab. Kundi hili linajaribu kudhibiti mkoa wa Cabo Delgada kutokana na utajiri wake mkubwa katika mafuta.

Joao Cravinho, Waziri wa Ulinzi, ambaye kwa sasa yuko Maputo, anataka kuanzisha makubaliano mapya ya ushirikiano wa ulinzi wa pande mbili.

Lisbon, ambayo itachukua uenyekiti wa Umoja wa Ulaya Januari 2021, inataka kuhamasisha nchi za Magharibi juu ya hali ya Msumbiji ambayo inatishia kanda nzima ya Afrika Mashariki, na inataka uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi ya kundi hili la kigaidi yamesababisha watu nusu milioni kuyatotroka makaazi yao ambao kwa sasa wanaishi katika hali duni zaidi na kusababisha vifo vya watu 2,000 katika kipindi cha miaka mitatu.