SUDAN-ETHIOPIA

Abdallah Hamdok na Abiy Ahmed waafikiana kuhusu mzozo wa Tigray

Waziri mkuu wa Sudani, Abdallah Hamdock
Waziri mkuu wa Sudani, Abdallah Hamdock ASHRAF SHAZLY / AFP

Baada ya mazungumzo kati ya Wazitri Mkuu wa SudanAbdallah Hamdok na mwenyeji wake wa Ethiopia, Jumapili Desemba 13, wawili hao wameafikiana kufanya mkutano wa dharura, utakaojumuisha mataifa yalio katika Jumuiya ya Maendeleo la Pembe ya Afrika IGAD, utakaohusu utatuzi wa mzozo wa Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Abdallah Hamdok amekuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea Ethiopia, tangu kuzuka kwa mapigano Novemba 4, ambayo yamezusha janga la kibinaadamu.

Ofisi ya Hamdok ilisema ziara hiyo inaongozwa na mazungumzo yenye tija na kwamba imekubaliwa kufanyika kwa mkutano wa dharura wa mataifa yalio katika Jumuiya ya Maendeleo la Pembe ya Afrika IGAD.

Hata hivyo ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia haijathibitisha tangazo la Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok.

Wakati huo Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu huyo wa Ethiopia inaeleza upande wa Sudan umeonesha uungaji mkono kwa serikali ya Ethiopia, katika jitihada zake za kusimamia utekelezwaji wa sheria za nchi.