COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d’Ivoire: Rais Ouattara ataapishwa kuwa rais kwa muhula wa tatu

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara Press Service of the Presidency/Handout via REUTERS

 Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara amekuwa rasmi rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu. Alassane Ouattara ameapishwa kwa muhula wa tatu kama rais wa nchi. Sherehe za kuapishwa kwake ilifanyika katika ikulu ya rais huko Abidjan.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe zimemalizika mapema alasiri. Wageni kisha wakaanza kuondoka ikulu ya rais jijini Abidjan. Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wamehudhuria hafla hiyo, ikiwa ni pamoja na rais wa Nigeria Mahamadou Issoufou, rais wa Togo Faure Gnassingbé, rais wa Ghana Nana Akufo-Addo na rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré.

Ufaransa iliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian. Rais wa zamani Nicolas Sarkozy pia amehudhuria sherehe hizo.

Akilihutubia taifa, rais Alassane Ouattara amewashukuru viongozi wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake na waalikwa wengine bila kusahau raia wa Côte d’Ivoire waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura akisema wote ni wananchi wa Côte d’Ivoire.

Wakati huo huo rais Ouattara ametangaza kuweka katika siku zijazo Wizara ya maridhiano ya kitaifa.

Rais wa Côte d’Ivoire pia amemtaka Waziri wake Mkuu, Hamed Bakayoko, kuanza tena majadiliano na vyama vya siasa kwa nia ya kufanya uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha miezi mitatu mwaka ujao:

"Ninaalika vyama vyote vya siasa kuchukua fursa hii ”, ametangaza Alassane Ouattara.