DRC

DRC: Mjane wa Jenerali Delphin Kahimbi kizuizini nyumbani

Kinshasa
Kinshasa Junior D. Kannah / AFP

Kulingana mjane wa Jenerali Delphin Kahimbi, mahakama ya kjeshi ilichukua uamuzi wa kumuweka katika kifungo cha nyumbani siku moja baada ya kuzikwa kwa mumewe, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Delphin Kahimbi alifariki dunia mwishoni mwa mwezi Februari katika hali mazingira ya tatanishi.

Siku chache baada ya mazishi ya mumewe Jumapili Desemba 8 huko Kiniezire, wanaume wanane waliovaa sare ya jeshi wakidai kuwa ni majaji wa mahakama ya kijeshi walifika nyumbani kwake Jumanne Desemba 10 na kumpa hati inayoeleza kwamba amewekwa katika kifungo cha nyumbani yeye na mama yake, amesema Brenda Kahimbi, mjane wa Jenerali Delphin Kahimbi, huku akibaini kwamba hajui sababu za uamuzi huo.

Inariptiwa kwamba uchunguzi bado unaendelea kubaini mazingira halisi ya kifo cha Jenerali Kahimbi. Rais wa Jamhuri, akinukuliwa katika ripoti ya Baraza la Mawaziri, anadai kuwa kunauwezekano kuwa jenerali Kahimbi huenda 'aliuawa kwa kunyongwa', baada ya dadili za kunyongwa kuonekana kwenye mwili wake.

Lakini mjane wake Brenda Kahimbi, hivi karibuni aliwaambia waandishi wa habari kwamba jenerali huyo alikufa kwa mshtuko wa moyo. Mahakama ya kijeshi bado haijamsikiliza Brenda Kahimbi, ambaye anafikiria kumtuma wakili wake kujibu wito wa tume ya uchunguzi.

Mahakama ya kijeshi bado haijatoa matokeo ya vipimo vya mwili wa jenrali Kahimi, ikisema inasubiri ripoti ya mwisho ya uchunguzi.