UN-DRC

Mkuu wa operesheni za kulinda amani za UN ziarani DRC

Jean-Pierre Lacroix, mjumbe wa katibu mkuu wa UN kuhusu operesheni za kulinda amani
Jean-Pierre Lacroix, mjumbe wa katibu mkuu wa UN kuhusu operesheni za kulinda amani UN Photo/Eskinder Debebe

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Jean-Pierre Lacroix anaanza ziara ya siku tano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mnamo Desemba 14.

Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Lacroix atakutana kwa mazungumzo na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO.

Ziara hii ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani nchini DRC, ilipangwa kwa wiki kadhaa, na kuahirishwa kwa baada ya Jean-Pierre Lacroix, kujiweka karantini. Hi ni moja wapo ya ziara za kawaida za mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Baada ya kuwasili Jumapili jioni Desemba 13, anatarajia kubaki siku mbili huko Kinshasa, kabla ya kuelekea mashariki mwa nchi, katika miko ya Kivu Kaskazini na Ituri, na kubaki huko kwa muda wa siku tatu.

Katika ziara yake hiyo nchini DRC, Jean-Pierre Lacroix atajadili na viongozi wa MONUSCO kuhusu tume hiyo, wakati muhula wake unatarajiwa kuongezwa muda Ijumaa 18 Desemba.

Jean-Pierre Lacroix pia atakutana na mashirika yasiyo ya kiserikali, baadhi ya wajumbe mashirika ya kiraia, na watu waliotoroka makazi yao, wakati mabadiliko ya ujumbe wa UN.

Hayo yanajiri wakati DRC inakabiliwa na mzozo wa ndani kati ya muungano wa kisiasa FCC na CASH, baada ya rais Etienne Tshisekedi kuvunja muungano huo Jumapili Desemba 6.