SUDAN-MAREKANI-UGAIDI

Sudan yaondolewa rasmi kwenye orodha nyeusi ya Marekani

Waziri Mkuu wa Sudan  Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok AP / File Photo

 Marekani imeiondoa rasmi Sudan kwenye orodha yake ya nchi zinazounga mkono ugaidi, hatua ambayo imechukuliwa leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Sudan kuwa wenye orodha hii kulizuia nchi za kigeni kufanya biashara na kuwekeza nchini humo kwa kuogopa vikwazo.

Sudan iliwekwa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi tangu mwaka 1993, ubalozi wa Marekani jijini Khartoum umetangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Wakati kipindi cha siku 45 cha taarifa kwa Bunge kimeisha, KWaziri wa mambo ya Nje wa Marekani ametia saini taarifa ya kuindoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi. Hatua hiyo inaanza kutumika Desemba 14," chanzo kimeongeza.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amebaini kwamba kuondolewa rasmi kwa Sudan kwenye orodha nyeusi ya Marekani ni "mabadiliko ya kimsingi" katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

"Tunakaribisha ujasiri wa wananchi wa Sudan kwa kutetea uhuru, amani na haki na tunawapongeza wajumbe wa serikali ya mpito inayoongozwa na raia kwa ujasiri wao katika kujibu matakwa ya raia wenzao," Mike Pompeo amesema katika taarifa.

Marekani ilichukua uamuzi wa kuiweka Sudan kwenye orodha yake nyeusi baada ya kumtuhumu rais wa Sudan wa wakati huo Omar al-Bashir kuwa na uhusiano na "makundi ya kigaidi", ikiwa ni pamoja na kundi la Al-Qaeda, ambalo kiongozi wake Osama Bin Laden aliishi katika nchi hii katika miaka ya 1990.