ETHIOPIA

Mgogoro wa Ethiopia: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lagawanyika

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS

Mvutano kati ya Ethiopia na Umoja aw Mataifa unaendelea kuhusu hali inayojiri katika imbo la Tigray: licha ya mazungumzo yanayoendelea, jamii ya kimataifa inashindwa kuishawishi serikali ya Ethiopia kuiruhusu itoe misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo kumejitokeza mgawanyiko katika Baraza la Usalama lenyewe, ambalo lilikuwa likikutana kwa mara ya pili juu ya suala hilo tangu mwishoni mwa mwezi Novemba.

 

Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanapingana juu ya jinsi ya kushinikiza Addis Ababa.

 

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifaamebaini kwamba shirika hilo limesikitishwa kwa kuwa bado halijafanikiwa kuingia katika jimbo la Tigray kutoa misaada ya kibinadamu, mwezi na nusu baada ya kuzuka kwa Operesheni ya jeshi la Ethiopia katika jimbo hilo.

 

Siku zinakwenda, wakati watu wanaohitaji misaada wanaendelea kukabiliwa tu na mateso, kulingana na Umoja wa Mataifa. Huko New York, wamebaini kwamba kambi za wakimbizi zitakosa chakula mwishoni mwa juma hili.

 

Umoja wa Mataifa unalaumu kwamba makubaliano ya kuingizwa misaada katika jimbo la Tigray, waliofikia na serikali, hayakuheshimishwa.